Mteule wa Rais Kagame akataliwa nchini Ubelgiji

KIGALI/BRUSSELS-Jamhuri ya Rwanda imesema inaichukulia hatua Serikali ya Ubelgiji kwa kukataa kuidhinisha uteuzi wa balozi wake, Vincent Karenga.

Msemaji wa Serikali ya Rwanda,Yolande Makolo amenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari akisema kuwa, hilo ni jambo la kusikitisha na ni uamuzi ambao hauna ishara nzuri kwa uhusiano wa nchi hizo mbili.

Balozi Karega ambaye amewahi kuhudumu katika nafasi ya Ubalozi wa Rwanda nchini Afrika Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo alifukuzwa Oktoba, mwaka jana wakati wa fukuto la mzozo kati ya Rwanda na DRC.

Aidha, Vincent Karega ambaye aliteuliwa kuwa balozi mpya wa Rwanda na Rais Paul Kagame mwezi Machi alitarajiwa kuchukua nafasi ya Dieudonné Sebashongore, ambaye ameshikilia wadhifa huo tangu 2020.

"Inasikitisha kwamba Serikali ya Ubelgiji inaonekana kuwa imekubali shinikizo kutoka kwa Serikali ya DRC na propaganda kutoka kwa mashirika na wanaharakati wanaopinga.Hii haijakaa vyema kwa mahusiano ya pande mbili baina ya nchi zetu,"Yolande Makolo alibainisha.

Aidha, ingawa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ubelgiji haijatoa tamko lolote kuhusiana na hatua hiyo, baadhi ya vyombo vya habari nchini Rwanda vimebainisha kuwa,kuna shinikizo kutoka mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini humo ambayo yameshinikiza kukataliwa kwa mteule huyo wa Rais Kagame.

Moja wapo ya sababu kuu ni tuhuma za Balozi Karega wakati akihudumu nchini Afrika Kusini na DCR kuwatendea ndivyo si vyi wapinzani wa utawala wa Rwanda.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news