Neema zaidi inakuja-Dkt.Mwinyi

PEMBA-Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 ndani ya kipindi cha miaka miwili na nusu tayari miradi mingi ya maendeleo imekamilika.

Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amesema kwa sasa ni kuendelea kuongeza juhudi zaidi kwenye kuimarisha sekta ya miundombinu ikiwemo barabara zitakazotumika zaidi ya miaka 60 mbele, ujenzi wa uwanja wa ndege wa kisasa Pemba, utakaojumuisha barabara ya kilomita 2.5.

Sambamba na jengo jipya la abiria ili kukifungua Kisiwa cha Pemba kwa uwekezaji, utalii na kutoa ajira mpya kwa wananchi.

Ameyasema hayo wakati akizungumza katika mkutano wake na mabalozi,wajumbe Halmashauri za CCM majimbo, wilaya na mkoa katika Ukumbi wa Umoja ni Nguvu uliopo Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba kwa ziara ya kichama na kukagua mali za CCM.

Makamu Mwenyekiti wa CCM, Dkt.Mwinyi ameahidi ujenzi wa kumbi za mikutano za kisasa kwa Unguja na Pemba zenye uwezo wa kubeba mikutano mikuu ya chama kitaifa.

Wakati huo huo,Makamu Mwenyekiti, Dkt.Mwinyi amemuagiza Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar, Dkt. Mohammed Said Dimwa kuanza kutoa vitambulisho vya mabalozi kwa ajili ya utaratibu wa malipo ya posho ya kujikimu kwa mwezi kwa mabalozi hao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news