Rais Dkt.Mwinyi azindua Bima ya Takaful

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, uanzishwaji wa huduma mpya ya Bima ya Takaful ni hatua muhimu katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za bima kwa wananchi ili kuchochea maendeleo ya Shirika la Bima Zanzibar (ZIC).

Ameyasema hayo Julai 5, 2023 alipozindua kampuni tanzu ya ZIC Takaful ambayo ni kampuni inayotoa huduma za bima kwa kufuata misingi na sheria za dini ya Kiislamu iliyoanzishwa na Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC).

Rais Dkt.Mwinyi amesema kuwa, kupitia wataalamu wa bima Takaful ni kiungo muhimu katika ukuaji wa huduma za fedha zinazofuata misingi ya Kiislamu kwa sababu huduma hiyo hutoa fursa kwa mabenki ambayo tayari yanaendeshwa kwa misingi hiyo kuweza kutoa huduma za bima jambo halikuwezekana kabla ya uanzishwaji wa Takaful.

Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi pia amewakaribisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuchangamkia fursa kuja kuwekeza katika huduma za bima za aina hii ya Takaful ili waweze kuongeza uwezo wa kukatia bima miradi mikubwa itakayochochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news