Serikali haitamsamehe yeyote-Dkt.Msonde

NA JAMES MWANAMYOTO
OR-TAMISEMI 

NAIBU Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt.Charles Msonde amesema, Serikali haitamsamehe yeyote atakayebainika kukwamisha ujenzi wa miundombinu ya elimu katika shule za sekondari na msingi.
Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde akikagua uimara wa ukuta wa darasa linalojengwa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Tinde, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Dkt.Msonde amesema hayo kwa nyakati tofauti akiwa wilayani Msalala,Ushetu na Kahama Manispaa kukagua utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya miundombinu ya shule za msingi na sekondari katika halmashauri hizo. 

“Serikali haitomsaheme yeyote atakayesababisha wanafunzi wakose mabweni na madarasa wakati imetoa kwa wakati fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hiyo ya elimu,”amesisitiza Dkt. Msonde. 
Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde akisisitiza jambo kwa walimu Shule ya Msingi Mtakuja na watendaji wa Manispaa ya Kahama alipowasili katika shule hiyo ya Mtakuja kwa ajili ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya elimu shuleni hapo.

 Aidha, ili kuhakikisha miundombinu ya elimu inakamilika kwa wakati, Dkt.Msonde amezitaka menejimenti za halmashauri hizo kuongeza mafundi wenye uwezo wa kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya elimu katika shule za sekondari na msingi ili wanafunzi wapate mazingira bora ya kupata elimu. 
Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde akihimiza jambo kwa walimu wa Shule ya Msingi ya Segesa ya wenye uhitaji maalum na watendaji wa Manispaa ya Kahama, mara baada ya kuwasili shuleni hapo kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo.

Ameongeza kuwa, ujenzi wa miundombinu hiyo ya elimu kupitia Mradi wa BOOST ilikuwa imepewa muda maalumu wa kukamilika, hivyo amewataka viongozi wa halmashauri zote nchini kuhakikisha ndani ya siku 10 wanakamilisha miundombinu hiyo ili iweze kutumiwa na wanafunzi.
Mwonekano wa madarasa yanayoendelea kujengwa katika Shule ya Msingi Bulyanhulu iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Msalala.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga ambaye ni Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Bi.Dafroza Ndalichako amesema, ofisi yake itahakikisha watendaji wa halmashauri zote zinazoteleza Mradi wa BOOST katika eneo lake la utawala, wanafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya elimu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news