Vyama vipya 18 vya siasa vyaomba usajili

DAR ES SALAAM-Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amesema vyama vipya vya siasa 18 vimeomba usajili ambapo utaanza kutekelezwa baada ya kuhitimishwa zoezi la uhakiki wa vyama vilivyopo.
Jaji Mutungi ameyasema hayo leo Julai 17, 2023 jijini Dar es Salaam katika mkutano wa kikao kazi na viongozi wa vyama vya siasa nchini.

Mkutano huo ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea kwenye uhakiki ambapo amesema hawezi kusajili vyama vipya kabla ya kufanyika uhakiki kwa vyama vilivyopo. Uhakiki wa vyama unatarajiwa kufanyika Julai 20, mwaka huu.

Amesema, wanaotaka kufuta hati chafu ambazo zimekuwa zikijitokeza kwa kuhakikisha vyama vinakuwa na wataalamu wa fedha ambao watakuwa wanafanya shughuli kwa kuzingatia weledi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news