CCM Zanzibar itajiendesha kiuchumi-Dkt.Mwinyi

PEMBA-Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameahidi kukisimamia CCM ili kijiendeshe kiuchumi Zanzibar.

Ameyasema hayo Julai 16,2023 kwenye mkutano wake na Mabalozi, Wajumbe wa Halmashauri za CCM Majimbo, Wilaya na Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati akihitimisha ziara yake ya kichama katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete na kutembelea mali na miradi mbalimbali ya CCM na Jumuiya zake Mkoa wa Kusini na Kaskazini Pemba.

Aidha, Makamu Mwenyekiti Dkt.Mwinyi amesema, chama lazima kuwekeza kiuchumi na kuwa na vitega uchumi vingi kama sehemu ya mapato yake kwa kuendelea kuboresha na kuwapatia maslahi bora watendaji wake wa ngazi zote .

Vilevile, alieleza kufurahishwa na rasilimali za chama kwenye ziara zake mikoa yote kichama Unguja na Pemba na kuelekeza kuzifanyia tathmini kuangalia uwezekano wa kuziendeleza kiuchumi pia kwa kushirikiana na sekta binafsi kuwekeza ili kuziimarisha zaidi na kuongeza mapato ndani ya chama.

Kwa upande mwingine Makamu Mwenyekiti Dkt.Mwinyi ameahidi ujenzi wa kumbi kubwa za mikutano mikuu ya chama kwa Unguja na Pemba, ujenzi mpya wa ofisi za chama zenye hadhi za juu pamoja na vitendea kazi vya ofisini zikiwemo kompyuta na vifaa vyote vya ofisi

Ziara ya Kaskazini Pemba imekamilisha ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt.Mwinyi na kwa kutembelea rasilimali za chama hicho zikiwemo majengo na vitega uchumi vyake kwa Mikoa yote mitano ya Unguja na Pemba kichama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news