Waziri Mkuu atoa siku saba kwa TARURA, DAWASA kukamilisha Barabara ya Muhimbili

DAR ES SALAAM-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewapa siku saba Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Dar es Salaam, Godfrey Mikinga na Mkurugenzi wa Usafi wa Usimamizi wa Usafi wa Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingiza (DAWASA), Lydia Ndibalema wawe wamekamilisha kipande cha barabara ya Mariki kinachoingia geti kuu la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kiwango cha lami.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua barabara ya Maliki inayounganisha Barabara ya Umoja wa mataifa na Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam, Julai 24, 2023. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila. Na kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini Mkoa wa Dar es salaam, Godfrey Mkinga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Barabara hiyo ambayo ilibomolewa kwa urefu wa mita 60 kupisha matengenezo ya bomba la maji machafu linalotoka katika hospitali hiyo ilipaswa kuwa imekamilika mwishoni wa mwezi wa sita 2023.

Mheshimiwa Majaliwa amewaagiza watendaji hao kufanya kazi usiku na mchana ili kuepusha adha kwa wagonjwa na wanafamilia wanaoitumia barabara hiyo kuelekea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mheshimiwa Majaliwa ametoa maagizo hayo leo Julai 24, 2023 alipofanya ziara ya kushitukiza kukagua barabara hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news