Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 24, 2026

Soma habari zote muhimu leo Oktoba 24, 2026 kutoka katika magazeti makubwa ya Tanzania kama Mwananchi, HabariLeo, Majira, Nipashe, Zanzibar Leo, Raia Mwema, Mwanahalisi, Uhuru, Pambazuko, Jamhuri na mengineyo kila siku bila malipo.
MWANANCHI - Jumamosi, Oktoba 24, 2026 habari kuu ni Sakata la Mwabukusi mtihani mahakamani ambapo Mawakili waeleza kushangaa Kamati ya Mawakili kuendelea na shauri dhidi yake wakati kuna amri ya kulisitisha kwa muda. Habari nyingine zilizopewa kipaumbele ni Takwimu saratani ya matiti zapaa nchini, Mapinduzi ya elimu: Vitabu vya sekondari vyaingizwa kwenye mfumo wa digitali, Mitihani ya marudio Chuo Kikuu Dar yaibua mjadala, na Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Denzel Trainer.
Zanzibar Leo - Jumamosi, Oktoba 24, 2026, Dk. Mwinyi kuingia mikataba ya kiutendaji na Mawaziri, Dk. Mkuya aonya udhalilishaji, ukatili kijinsia Vyuo Vikuu, Katibu Mkuu UN atoa wito kukomeshwa vita, Miradi ujenzi wa barabara ikamilike kwa wakati - Balozi Omar, Masauni: Tanzania kuwa kitovu soko la biashara ya kaboni Afrika na Mazrui abainisha ukubwa wa saratani ya matiti.

Zanzibar Leo Michezo - Jumamosi, Oktoba 24, 2026, Yanga SC, TRA United vita ya kibabe, Ibenge ataka ushindi dhidi ya ZED FC, Bodi ya Ligi yaikamua Simba 15m/- na Asia sasa yamuunga mkono Infantino.
Taifa Tanzania - Jumamosi, Oktoba 24, 2026, Taasisi 2,682 zaanza kutumia nishati safi ya kupikia, Serikali yalenga taasisi 30,000, El Nino kuathiri mvua za msimu 2026/2027, Chalamila aitaka TBA kushirikiana na sekta binafsi kufanya uwekezaji, Tanzania yaazimia kuwa wazalishaji chakula 10 bora duniani, na Mradi wakukuza soko la bidhaa za kikolojia kunufaisha wakulima.

Taifa Tanzania Michezo - Jumamosi, Oktoba 24, 2026, AZAM KUSAKA USHINDI KOMBE LA SHIRIKISHO, MASHABIKI 3,000 KUINGIA BURE LEO, Mashabiki waiponza Simba SC, yapigwa faini Sh. Mil. 15, TRA yaapa kuichapa Young Africans leo, na Pamba yawabana Polisi kwao, yatoka sare 1-1.
Nipashe - Jumamosi, Oktoba 24, 2026, MGOGORO DALADALA NA BAJAJI MBEYA Madereva 34 waenda jela, Vurugu, maandamano yasiyo halali yawaponza, Kamanda Kuzaga aonya madereva wasiotii sheria, EAC yapewa magari 16 kuimarisha usalama wake, Watu watano wakamatwa wakidaiwa kufanya mauaji, Utaratibu mpya mitihani 'sup' waibua mjadala wasomi UDSM, Nchi 20 kukutana Dar es Salaam kujadili ufadhili wa elimu na Saudi Arabia yazidi kushambuliwa.

Michezo Nipashe - Jumamosi, Oktoba 24, 2026, Manqoba ataja siri tatu za ushindi, Ni katika mechi ya Ligi Kuu dhidi ya TRA United, ingawa anakiri ina nyota na SIMBA YASAKA REKODI CAF.
WAMACHINGA - Jumamosi, Oktoba 24, 2026, TMA yatabiri mvua kubwa za El Niño kuanzia Novemba hadi Aprili huku ikionya kuhusu uwezekano wa mafuriko, magonjwa na uharibifu wa miundombinu, Dkt. Chang'a aeleza athari zaidi mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Singida, Dodoma, Njombe, Iringa, Mbeya, Songwe na Rukwa pamoja na maeneo ya kusini mwa Morogoro yakiwa hatarini, huku habari nyingine zilizopewa kipaumbele zikiwa Mwigulu: Tanzania inajipanga kulisha Dunia na Samia ateua vigogo TAWA, TTB na TANAPA.

WAMACHINGA Spoti - Jumamosi, Oktoba 24, 2026, Yanga yaonyesha ukomavu kwa Sure Boy, Azam, Singida BS zapania makundi, Lewis Hamilton aiombea Congo DR, Makoena atajwa moja ya makocha bora na, Karia: TFF sasa kuwapima Wachezaji.
MwanaHabari - Jumamosi, Oktoba 24, 2026, Tanzania yalenga kuwa mzalishaji bora wa chakula duniani, Waziri Mkuu asema ni kuwa miongoni mwa wazalishaji 10 bora na kinara wa uzalishaji chakula barani Afrika, ikimarisha uwekezaji katika kilimo, sayansi na teknolojia ili kuongeza uzalishaji na kupanua masoko ya ndani na nje ya nchi. Habari nyingine zikiwa TMA yatahadharisha magonjwa ya mlipuko, mafuriko mvua za El Nino, SMZ yataka vitabu vya ziada viwekwe kidigitali, vizingatie utamaduni wa visiwa hivyo, Kiliba: Napambana na wanaomtukanana Rais na kubeza kazi anazofanya na Naibu Waziri Londo aahidi kufuatilia changamoto za viwanda kukuza uzalishaji wa ndani.

MwanaHabari Michezo - Jumamosi, Oktoba 24, 2026, Simba yawaita mashabiki kumalizana na De Agosto kesho, huku habari nyingine zikiwa Tusker yaanza safari kuifuata Singida BS, Hamilton ataka Dunia kuikomboa Congo DR, Ibenge: ZED ni washindi wazuri na Rooney amshambulia Nahodha Man U.
MWANA SPOTI - Jumamosi, Oktoba 24, 2026, MITIHANI MIWILI YANGA, Manqoba ana kazi ngumu kuibeba CAF. BARKER AWAONYA MASTAA, Simba vs Agosto 2nd Leg Jumapili saa 10:00 jioni huku Simba ikiwa imewahi kufika nusu fainali ya kombe la mabingwa mwaka 1974, AZAM ndani ya presha ya CAF dhidi ya ZED FC saa 10:00 jioni Azam Complex, na Ligi Kuu Bara leo Jumamosi JKT Tanzania vs Kagera saa 12:00 jioni Isamuhyo.
UHURU - Jumamosi, Oktoba 24, 2026, Rais Mwinyi, mawaziri kuingia mikataba kazini, ni mfumo rasmi kuhakikisha ufanisi serikalini, watakaofanya vizuri 'kupewa maua', ukiboronga, huku habari nyingine zikiwa Tanzania, Marekani zajikita faida kiuchumi, Chatanda azidi kuchanja mbuga akimnadi Ndilito, CCM yakoshwa SMZ kuongeza mishahara na Usingizi 'dili' kubwa kiafya.

HabariLEO - Jumamosi, Oktoba 24, 2026, Mauaji yatikisa, Wanawake 2 wauawa gesti Mbeya, wafichwa uvunguni mwa kitanda; 5 wadakwa mauaji Tanga, Mtandao watetezi haki za binadamu waanika zaidi ya 1,600 wauawa, wanawake waongoza, huku habari nyingine zikiwa Tanzania yapania 10 bora uzalishaji chakula duniani, TMA YAONYA MVUA KUBWA, MAFURIKO, Awamu ya pili bima ya afya kwa wote yaanza kwa kasi, na DK Samia ateua wenyeviti wa bodi watatu.

HabariLEO Michezo - Jumamosi, Oktoba 24, 2026, Polisi yaanza kwa sare Ushirika, Polisi Tanzania imebanwa nyumbani na Pamba Jiji ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kutoka sare ya kutumana bao 1-1 kwenye Uwanja wa Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro, huku habari nyingine zikiwa Yanga kujijuliza kwa TRA United leo, Simba Yalimwa Faini Mil 15/-, na Eve Kupeperusha Bendera ya Tanzania Nigeria.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here