CCM yamteua Bahati Keneth Ndingo kugombea ubunge Mbarali

DODOMA-Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan imekutana katika kikao chake maalum kilichofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Agosti 17,2023.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi leo, Sophia Edward Mjema pamoja na mambo mengine, Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Bahati Keneth Ndingo kuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM katika Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya.

Ni kupitia uchaguzi mdogo wa ubunge uliopangwa kufanyika Septemba 19,2023, kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Francis Leonard Mtega aliyefariki dunia Julai Mosi, 2023.

Pia, kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kamati Kuu ya CCM imezipongeza Serikali zake zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

Ni kwa namna zinavyoendelea kuwatumikia wananchi kwa vitendo kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 hadi 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news