Dkt.Yonazi aongoza kikao cha Jimbo la Serikali

DAR ES SAALAAM-Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ameongoza kikao cha Jimbo la Serikali kilichofanyika tarehe 24 Agosti, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Serengeti uliopo Jengo la Ushindani jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati wa kikao cha Jimbo la Serikali kilichofanyika tarehe 24 Agosti, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Serengeti uliopo Jengo la Ushindani Dar es Salaam.

Kikao hicho kilihudhuriwa na wajumbe kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Wizara ya Fedha, Wizara ya Afya, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania(TACAIDS) pamoja na Bohari ya Dawa (MSD),
Baadhi ya Wajumbe wakifuatilia hoja wakati wa kikao cha Jimbo la Serikali kilichofanyika tarehe 24 Agosti, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Serengeti uliopo Jengo la Ushindani Dar es Salaam.

Kikao hicho kililenga kujadili utekelezaji wa Programu za Malaria, UKIMWI, Kifua Kikuu, na Uimarishaji wa Mifumo ya Utoaji Huduma za Afya nchini kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia (Global Fund). 
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali ofisi hiyo Bw. Paul Sangawe wakipitia nyaraka za kikao cha Jimbo la Serikali kilichofanyika tarehe 24 Agosti, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kililenga kujadili utekelezaji wa Programu za Malaria, UKIMWI, Kifua Kikuu, na Uimarishaji wa Mifumo ya Utoaji Huduma za Afya nchini kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia (Global Fund).
Mkuu wa Program Wizara ya Afya Dkt. Catherine Joiachim akizungumza jambo wakati wa kikao cha Jimbo la Serikali kilichofanyika tarehe 24 Agosti, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Aidha, kikao hicho ni sehemu ya maandalizi ya kikao cha Tanzania National Coordinating Mechanism (TNCM) ambacho wajumbe wake ni Jimbo la Serikali, Asasi za Kiraia (NSA), na Wadau wa Maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news