FIFA,TFF waifungia Yanga SC

DAR ES SALAAM-Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limeifungia Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam kufanya usajili hadi hapo itakapomlipa aliyekuwa kiungo wake,Gael Bigirimana.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Agosti 29,2023 na Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikiso la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),Cliford Mario Ndimbo.

"Klabu ya Young Africans iliyo Ligi Kuu ya NBC imefungiwa kusajili mpaka itakampolipa mchezaji Gael Bigirimana.

"Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya mchezaji huyo kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo. Birigimana alifungua kesi FIFA kuhusiana na malipo ya ada ya usajili (sign on fee),"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Yanga SC ilitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo.

Wakati FIFA imeifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa wachezaji Kimataifa, Shirikiso la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeifungia kufanya uhamisho wa ndani.

"TFF inazikumbusha klabu kuheshimu mikataba ambayo zimeingia na wachezaji pamoja na makocha ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili.

"Iwapo klabu inataka kuvunja mkataba na wachezaji au kocha, inatakiwa kufanya hivyo kwa kuzingatia taratibu,"imefafanua taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news