JKT Tanzania yajuta kukutana na Yanga SC, yatandikwa mabao 5-0

DAR ES SALAAM-Mabingwa wa Tanzania, Yanga SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kuitandika JKT Tanzania mabao 5-0.

Ni kupitia mtanage wa nguvu uliopigwa usiku wa Agosti 29,2023 ndani ya Uwanja wa Azam Complex uliopo Kata ya Chamazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Stephane Aziz Ki dakika ya 46,Kennedy Musonda dakika ya 54,Kouassi Attohoula Yao dakika ya 64 na Max Mpia Nzengeli dakika ya 79 na 88.

Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha alama sita na kupanda kileleni ikizizidi wastani wa mabao Azam FC na Simba SC baada ya wote kucheza mechi mbili, wana Jangwani wakijiwekea rekodi ya kipekee kuvuna mabao 10 kwenye mechi mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news