Hizi hapa bei za mafuta mwezi Agosti 2023, zingatia mambo haya

DAR ES SALAAM-Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),Dkt. James A.Mwainyekule ametangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano, tarehe 2 Agosti 2023 saa 6:01 usiku.
Ameeleza kuwa, kwa mwezi Agosti 2023, bei za rejareja za mafuta katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ni kama ifuatavyo:

Mkoa wa Dar es Salaam mafuta ya Petroli yanauzwa kwa shilingi 3,199 huku Diezeli ikiuzwa kwa shilingi 2,935 na mafuta ya taa lita yanauzwa kwa shilingi 2,668.

Kwa upande wa Mkoa wa Tanga mafuta ya Petroli yanauzwa kwa shilingi 3,245 huku Diezel 2,981 ikiuzwa kwa shilingi na mafuta ya taa yanauzwa kwa shilingi 2,740.

Dkt.Mwaunyekule ameeleza kuwa, kwa upande wa Mkoa wa Mtwara mafuta ya Petroli yanauzwa kwa shilingi 3,271 huku Diezeli ikiuzwa kwa shilingi 3,008 na mafuta taa kwa shilingi 2,714.

Pia, amesema mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Agosti 2023 yanatokana na changamoto za upatikanaji wa Dola za Marekani, mabadiliko ya sera za kikodi, kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani, ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia na gharama za uagizaji wa mafuta.

Bei za mafuta katika miji,wilaya na mikoa ni kama zinavyooneshwa katika Jedwali Na. 1 na bei za mafuta kwa
wafanyabiashara wa jumla ni kama zinavyooneshwa katika Jedwali Na. 2.

EWURA imebainisha kuwa, wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei
zinazooneshwa katika Jedwali Na. 1.

Aidha, wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali Na. 2.

Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka AGIZO hili.EWURA inapenda kuwakumbusha wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla na rejareja pamoja na jamii kuzingatia yafuatayo: -

a) bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo.Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini.

b) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta.

c) Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani isipokuwa bei hizo zisizidi bei kikomo (Price cap) au kuwa chini ya bei iliyoruhusiwa (Floor Price) kama zilivyokokotolewa kwa mujibu wa Kanuni za EWURA za Kupanga Bei za Mafuta za Mwaka 2023 zilizotangazwa kupitia Gazeti la Serikali Na. 421 la tarehe 23 Juni 2023.

d) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana yakionesha bei za mafuta, punguzo, vivutio vya kibiashara vinavyotolewa na kituo husika.

Pale ambapo inawezekana kuchagua,wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta
kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani.

Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja. Adhabu kali itatolewa kwa
kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika.

e) Wauzaji wa bidhaa za mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa stakabadhi za mauzo kutoka kwenye Electronic Fiscal Pump Printers (EFPP) na wanunuzi wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita.

Stakabadhi hizo zitatumika kama kidhibiti kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora unaotakiwa.

Stakabadhi hizo pia zitasaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na mauzo ya bidhaa za mafuta ya petroli.

JEDWALI 1: BEI KIKOMO ZA REJAREJA KWA SHILINGI/LITA





Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news