Huu ni ukurasa mpya wa maendeleo Sekta ya Michezo-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Agosti 27, 2023 Zanzibar imefungua ukurasa mpya wa maendeleo ya sekta ya michezo kwa kuzindua rasmi mchezo wa ngumi.
Masumbwi yamezinduliwa kuwa miongoni mwa michezo iliyoruhusiwa kuchezwa Zanzibar kama ilivyo michezo mingine kwa kuzingatia sheria na kanuni za mchezo huo kimataifa. 
Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo wakati akizindua rasmi mchezo wa ngumi za kulipwa Zanzibar uliyoshirikisha mabondia kutoka Tanzania Bara na Zanzibar uliofanyika uwanja wa Mao Tse Tung, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa, uamuzi wa Serikali kuruhusu mchezo wa ngumi Zanzibar umetokana na maoni ya wananchi wengi kutaka mchezo huo uruhusiwe. 
Pia, amesema haikuwa kazi nyepesi kuurudisha mchezo huo baada ya kuzuiwa kwa zaidi ya miaka 50.

Vilevile, mchezo wa ngumi ni fursa nyingine ya vijana wa Zanzibar kunufaika katika sekta ya michezo na kuweza kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa ya mchezo wa ngumi .
Kwa upande mwingine mchezo huo utaweza kuitangaza Zanzibar na kuchochea utalii kupitia sekta ya michezo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news