Kocha Hans van der Pluijm atimuliwa Singida Fountain Gate

SINGIDA-Uongozi wa Singida Fountain Gate umeachana na Kocha wake Mholanzi, Hans van der Pluijm kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu tangu kuanza kwa msimu.

Hans van der Pluijm ambaye aliongeza mkataba mpya ikimaanisha mwaka mmoja alipomaliza Juni 30, mwaka huu imeonekana ufanisi hauridishi,kwani uongozi huo umefanya uwekezaji mkubwa kwa sasa.

Aidha,kocha msaidizi Mathias Lule anatarajiwa kuendeleza jukumu zito la timu hiyo ambayo kwa sasa inaendelea na michuano muhimu barani Afrika na Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Kocha huyo anaondoka akiwa ameiwezesha timu hiyo kumaliza nafasi ya nne na kufuzu michuano ya CAF na kufanikiwa kufuzu hatua ya kwanza Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Aidha, timu hiyo imetinga hatua hiyo baada ya kushinda mabao 4-1 dhidi ya JKU mchezo wa kwanza na kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa wapinzani wao.

Kuhusu timu hii

Klabu ya Singida Fountain Gate ilianzishwa mwaka 2010 ikiwa ni timu ya wafanyakazi wa Benki ya DTB ikifahamika kwa jina la DTB Football Club kabla ya kubadilishwa jina.

DTB FC baadae ilipata hamasa kubwa baada ya kushiriki mabonanza ya mabenki nchini na kufanya vizuri, hivyo kupelekea uongozi wa DTB kuwekeza kwenye timu na kuipeleka kushiriki michuano ya mashindano hadi kushiriki Ligi Daraja la Kwanza (Championship).

Baada ya kufanya vizuri kwenye championship na kufanikiwa kupanda daraja kwenda Ligi Kuu mwaka 2022, Benki ya DTB iliamua kutoendelea kumiliki timu ya mpira ili kubaki katika kazi zake za msingi za kibenki.

Hii ilitoa fursa kwa wadau kutoka mkoani Singida kuinunua timu hiyo na kuibadilisha jina kutoka DTB FC kwenda Singida Big Stars.

Mwaka 2022/2023, Klabu ya Singida Big Stars ilianza kushiriki Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara na kufanikiwa kufanya vizuri kutokana na mkakati wake wa kusajili wachezaji wa kimataifa wenye ubora wa hali ya juu.

Sambamba na wale waliocheza vilabu vikubwa vya Tanzania vikiwemo Simba, Yanga, Azam, Mtibwa, Mbeya City na kadhalika.

Mafanikio ya klabu ya Singida Big Stars yanatokana na ubora wa wachezaji, benchi la ufundi na uongozi madhubuti.

Baada ya kumalizika msimu wa 2022/23 kwa mafanikio makubwa, Klabu ya Singida Big Stars ilipata ofa nzuri kutoka kwa mwekezaji Fountain Gate Academy ambaye aliinunua kwa lengo la kuiboresha zaidi na kuiendesha kisasa.

Aidha, baada ya kununuliwa, Singida Big Stars ikatengeneza muunganiko na Fountain Gate Academy hatimaye kupata jina lake jipya la Singida Fountain Gate FC.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news