Kocha Mkuu wa Simba SC afunguka

MOROGORO-Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba,Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema, anaendelea kufanya mabadiliko ya kikosi mara kwa mara ili wachezaji waendelee kuzoeana.

Robertinho amesema katika mchezo wa Agosti 17, 2023 dhidi ya Mtibwa Sugar alifanya mabadiliko machache ya wachezaji kipindi cha kwanza kabla ya kuwaweka wazoefu cha pili na kubadili mchezo.

Aidha, Kocha Robertinho ameongeza kuwa, waliweza kucheza vizuri na kupata mabao mawili ya haraka kabla ya kupoteza umakini na kusababisha Mtibwa kusawazisha yote.

“Tunaendelea kufanya mabadiliko ya kikosi taratibu ili wachezaji wazidi kuzoeana.Tuna timu bora, lakini tunapaswa kucheza kitimu. Nawapongeza wachezaji wangu kwa ushindi huu,”amesema Robertinho.

Akizungumzia makosa ya kiulinzi yaliosababisha Mtibwa kusawazisha mabao mawili, Robertinho amesema, “unajua tunamkosa Henock Inonga ambaye ni mlinzi kiongozi.

“Henock alianza kuzoeana kiuchezaji na Che Fondoh Malone, lakini ameumia. Tunae Kennedy Juma na Hussein Bakari wanafanya vizuri, lakini wanapaswa kucheza pamoja mara kwa mara ili wawe bora zaidi,”amesema Robertinho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news