Mabasi ya Achimwene Safari yazinduliwa

MBEYA-Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Juma Zuberi Homera amezindua mabasi mapya ya kisasa Achimwene Safari.

Homera ameipongeza Kampuni ya Achimwene Safari kwa kuendelea kufanya uwekezaji huu mkubwa ndani ya Mbeya na Tanzania kwa sababu wanaendelea kumuunga mkono Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kukuza uchumi wa nchi.

Amezindua mabasi hayo Agosti 12,2023 huku akimpongeza sana Mkurugenzi wa kampuni hiyo,Heneriko Achimwene kwa uzalendo huo mkubwa, kwani vijana wanapata ajira.

Mhe.Homera amesema, Serikali ya Mkoa wa Mbeya itaendelea kuunga mkono jitihada za Kampuni ya Achimwene ili waendelee kuwekeza zaidi.

Pia amewaomba wana Mbeya na Watanzania kumuunga mkono mwekezaji huyo ili aendelee kuwekeza zaidi kwa maana mabasi hayo ni ya kisasa, yana choo ndani na yataepusha ajali na kupunguza usumbufu wa kushuka shuka kuchimba dawa.

Aidha, ametoa rai kwa madereva wote Tanzania kuendesha mabasi kwa kufuata sheria za barabarani kuepusha ajali zisizo za lazima, kwa wasiofuata sheria hizo na kusababisha ajali watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Achimwene, Heneriko Achimwene ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano mkubwa kwa wawekezaji, hali inayosababisha mpaka vijana wanaendelea kufanya uwekezaji kama huo.

Pia, mtendaji mkuu, Innocent Joseph amewashukuru watanzania wote kwa kuendelea kushirikiana na Kampuni ya Achimwene akisema mabasi hayo ni ya watanzania, safari zake ni kutoka Mbeya kwenda Dar es Salaam na kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya kila siku.

Katika hafla hiyo ya uzinduzi wa mabasi hayo mapya Achimwene Safari wadau mbalimbali walihudhuria akiwemo msanii wa kuigiza sauti za viongozi Oscar Nyerere kama balozi wa mabasi hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news