Mbunge CCM ajiuzulu

DODOMA-Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya (CCM),Mheshimiwa Bahati Keneth Ndingo amejiuzulu nafasi hiyo ili agombee ubunge wa Jimbo la Mbarali katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

Bahati amejuzulu nafasi hiyo kwa mujibu wa lbara ya 149 (1) (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Katika barua yake kwa Spika, ameeleza sababu za kujiuzulu ni kuangalia namna nyingine ya kuwatumikia Watanzania katika Bunge.

"Ninakusudia kushiriki kwenye mchakato wa Uchaguzi Mdogo wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Mbarali unaotarajiwa kufanyika siku za hivi karibuni,"imeeleza barua hiyo.

Hivi karibuni Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Bahati Keneth Ndingo kuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM katika Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya.

Ni kupitia uchaguzi mdogo wa ubunge uliopangwa kufanyika Septemba 19,2023, kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Francis Leonard Mtega aliyefariki dunia Julai Mosi, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news