Muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2023

DODOMA-Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti inawaalika wadau kutoa maoni kuhusu Muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2023 kwa mujibu wa Kanuni ya 97(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Februari, 2023.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Agosti 9,2023 na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa,Ofisi ya Bunge jijini Dodoma.

Mkutano wa kupokea na kusikiliza maoni ya wadau (Public Hearing) utafanyika siku ya Jumanne na Jumatano tarehe 15 na 16 Agosti, 2023 saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Ofisi ya Bunge jijini Dodoma.

Kamati inawaalika watu wote wenye maoni kuhusu Muswada huo kufika na kuwasilisha maoni yao kabla haujapelekwa katika hatua nyingine.

Vilevile Kamati itapokea maoni kwa njia ya posta au Barua pepe kwa
anuani ifuatayo:-
Katibu wa Bunge,
Ofisi ya Bunge,
10 Barabara ya Morogoro
S.L.P. 941,
40490 Tambukareli,
DODOMA.
Barua pepe: cna@bunge.go.tz na kamati@bunge.go.tz
Muswada huo pia unaweza kupakuliwa katika tovuti ya
Bunge, https://www.bunge.go.tz/bills-list.

Aidha, unashauriwa kuwasilisha jina lako kupitia barua pepe tajwa endapo utapenda kuwasilisha maoni
yako kwa kuzungumza kwa ajili ya hatua za kiutawala.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news