Simba SC yasema vibali vitakuwa tayari

DAR ES SALAAM-Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema, vibali vya wachezaji wote vitakuwa vimepatikana kabla ya kuanza mchezo wao dhidi ya Singida Fountain Gate FC.
Ahmed amesema, utaratibu wote umefanyika ilikuwa imebaki malipo ambapo kila kitu kitakaa sawa kabla ya mchezo huo wa Agosti 10,2023 Mkwakwani jijini Tanga.

Hayo yanajiri ikiwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kwamba ni Azam FC iliyowasilisha vibali vya wachezaji wake 10 wa kigeni kwa ajili ya kucheza michuano ya Ngao ya Jamii.
Michuano hiyo ya timu nne imeanza Agosti 9,2023 saa 1:00 usiku Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga,ambapo mabingwa watetezi Yanga wamefungua dimba na Azam FC.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news