Nimeridhika na thamani ya fedha zilizotumika hapa-Waziri Simbachawene

NA VERONICA MWAFISI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewapongeza viongozi na wananchi wa Kijiji cha Mwanangwa kwa kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo kikamilifu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoka kukagua Shule ya Sekondari ya Wasichana Mwanangwa iliyojengwa kwa ufadhili wa TASAF katika Kijiji cha Mwanangwa, wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Ni baada ya kuridhishwa na thamani ya fedha iliyotumika katika mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mwanangwa iliyojengwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza. 

Mhe. Simbachawene ametoa pongezi hizo alipokuwa akizungumza na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na wananchi wa Kijiji cha Mwanangwa, Kata ya Mabuki katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wakati wa ziara yake ya kikazi katika halmashauri hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa shughuli za TASAF. 
Muonekano wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mwanangwa iliyojengwa kwa ufadhili wa TASAF katika Kijiji cha Mwanangwa, Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

“Nimefurahi sana na niwapongeze kwa kusimamia kikamilifu mradi huu wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mwanangwa uliogharimu takribani shilingi milioni 168 kupitia fedha za TASAF, nimekagua na kuona majengo yote yalivyojengwa kwa ufanisi mkubwa, nimeridhika na thamani ya fedha ambayo imetumika hapa,’’ Mhe. Simbachawene amesema. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akimsikiliza Mkurugenzi wa Miradi ya Jamii-TASAF, Bw. John Stephen alipokuwa akifafanua jambo kwa Waziri huyo mara baada ya kukagua Shule ya Sekondari ya Wasichana Mwanangwa iliyojengwa kwa ufadhili wa TASAF katika Kijiji cha Mwanangwa, wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Aidha, Mhe. Simbachawene amewapongeza na kuwashukuru wananchi wa Misungwi kwa kuchangia nguvu zao katika kufanikisha ujenzi huo, hali inayoonyesha jamii pia imeshiriki kikamilifu katika ujenzi wa shule hiyo itakayowasaidia wanafunzi wa kike kupata elimu bora. 
Baadhi ya Wananchi na walengwa wa TASAF wa Kijiji cha Mwanangwa, Kata ya Mabuki wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akizungumza na Wananchi na walengwa hao wa TASAF mara baada ya kukagua Shule ya Sekondari ya Wasichana Mwanangwa iliyojengwa kwa ufadhili wa TASAF, wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe. Paulo Chacha amemshukuru Waziri Simbachawene kwa kufanya ziara katika Wilaya yake na kuahidi kuwa watumishi na wananchi wa Wilaya yake wataendelea kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano mkubwa ili kuleta maendeleo katika nchi. 

Naye, Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Mhe. Alexander Mnyeti amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwapatia fedha za miradi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi na vituo vya afya katika jimbo la Misungwi. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi na walengwa wa TASAF wa Kijiji cha Mwanangwa mara baada ya kukagua Shule ya Sekondari ya Wasichana Mwanangwa iliyojengwa kwa ufadhili wa TASAF, wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili katika Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba na Misungwi mkoani Mwanza iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF pamoja na kuzungumza na watumishi wa umma kwa lengo la kutatua kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi wa halmashauri hizo. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news