Prof.Janabi awauma sikio Wafamasia

DAR ES SALAAM-Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Mohamed Janabi amewataka wafamasia kuzingatia uaminifu pamoja na weledi katika utendaji kazi wao wa kila siku.
Prof. Janabi ameyasema hayo wakati wa hafla ya kuwapongeza wafanyakazi bora wa robo ya nne iliyoandaliwa na Idara ya Famasi MNH ambapo Wafamasia watatu Faraji Chambuso, Seleman Madebe na Scholastica Chimani walitunukiwa vyeti na zawadi.
"Maisha ni mbio ndefu (marathon) na mafanikio ni matokeo ya mchakato wa kitambo fulani, usijaribu kudhani maisha ni mbio ya mita mia kwa kujiingiza kwenye vitendo vya wizi wa dawa, hospitali haitavumilia mtumishi wa aina hii akikamatwa atawajibishwa ipasavyo," amesema Prof. Janabi

Aidha,amepongeza idara nzima ya famasi kwa kufanya kazi kwa bidii jambo ambalo limepelekea kupunguza changamoto ya upungufu wa dawa na kupunguza foleni kwenye madirisha ya dawa.
Awali akiwasilisha taarifa ya idara hiyo, Mkuu wa Idara hiyo,Mfamasia Nelson Njau alisema, idara imefanikiwa kuongea upatikanaji wa dawa kufikia asilimia 98, kupunguza gharama za ununuzi wa dawa ambapo katika kipindi cha miezi kumi imeokoa shilingi bilioni mbili. 

Ukililinganisha na vipindi vilivyopita, pamoja na kujifunza matumizi bora ya dawa za saratani jambo ambalo limesaidia kuokoa zaidi ya shilingi milioni 200.
"Tumeingia mikataba mbalimbali ya mashirikiano ikiwemo mkataba na Shirika la Direct Relief na hivi karibuni tunategemea kupokea msaada wa dawa zenye thamani ya shilingi bilioni moja. 

"Pamoja na mkataba na TMDA ambao matunda yake yameshaanza kuonekana hasa katika eneo la usalama wa dawa," amesema Mfamasia huyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news