Prof.Muhongo, Kamati ya Siasa wakagua miradi jimboni

NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Mheshimiwa Prof. Sospter Muhongo ameambatana na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Wilaya ya Musoma Vijijini kukagua miradi miwili ya maji ya bomba inayotekelezwa na Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi na Mazingira Vijijini (RUWASA) ambapo Utekelezaji wa miradi hiyo ni umetajwa kuwa ni mzuri.
Picha za zikionesha matukio mbalimbali ya ukaguzi wa miradi miwili ya maji ya Musoma Vijijini, na Maabara ya Bulinga Sekondari ya Kata ya Bulinga katika Jimbo la Musoma Vijijini.

Hayo yamebainishwa leo Agosti 8, 2023 kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, ambapo zoezi la kukagua miradi hiyo na kusikiliza kero za wananchi limefanyika Agosti 7, 2023.

"Jimbo la Musoma Vijijini lina kata 21, vijiji 68 na vitongoji 374. Vijiji vyetu vyote vina miradi ya maji ambayo iko kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji. Miradi ya maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria inatekelezwa kwa kasi kubwa jimboni kwetu."

Taarifa hiyo imefafanua kwamba, Mradi wa Kata ya Bwasi Vijiji vitakavyonufaika na upatikanaji wa maji ya bomba ya mradi huo ni Bwasi, Bugunda na Kome
na Chanzo cha maji kiko ziwani kwenye Kitongoji cha Bujaga Kijiji cha Bujaga, Kata ya Bulinga. Vijiji vitatu vya Kata ya Bulinga (Bujaga, Bulinga na Busungu) tayari vinapata maji ya bomba.

"Utekelezaji wa mradi huu, ujenzi wa tenki la ujazo wa lita 150,000, unakamilishwa. Lipo kwenye Kitongoji cha Rugongo, Kijijini cha Bwasi bomba kuu la kusambaza maji limetandazwa kilomita 18 kati ya 31.5 vituo vya kuchotea maji 25 kati ya 35 vimeishajengwa.

"Gharama ya mradi ni shilingi milioni 997.71 na mradi ulianza Februari 2023, utakamilishwa kabla ya tarehe Oktoba 30,2023,"imeeleza taarifa hiyo.

Mbali na mradi huo, mwingine ni Mradi wa Chumwi-Mabuimerafuru ambapo mradi huo unaanzwa kutekelezwa kwenye Vijiji vya Chumwi Kata ya Nyamrandirira na Mabuimerafuru Kata ya Musanja baadaye utapanuliwa na maji yatasambazwa kwenye vijiji vyingine vya kata hizo mbili.

"Utekelezaji wa mradi huu.Chanzo cha maji ya mradi huu kiko ziwani kwenye Kitoji cha Nyachumwi katika Kijiji cha Chumwi. Ujenzi wa tenki la ujazo wa lita 300,000 unakamilishwa liko kijijini Mabuimerafuru.

"Bomba kuu la kusambaza maji limetandazwa umbali wa kilomita 13 kati ya 24.24, Vituo vyote 17 vya kuchotea maji tayari vimejengwa.

"Aidha, gharama ya mradi ni Shilingi bilioni 1.6 mradi huu ulianza kutekelezwa Februari 2023, utakamilika kabla ya Oktoba 30,2023."

KUHUSU KERO NA MATATIZO YA WANAVIJIJI

Wanavijiji wamepata muda wa kutosha wa kuwasilisha kero na matatizo yao. Majibu yalitolewa na Mbunge wa jimbo, Prof. Sospeter Muhongo. Maswali yaliyohusu chama yalijibiwa na Mwenyekiti Denis Ekwabi na Katibu Valentine Maganga.

Aidha, kero na matatizo yaliyowasilishwa yamepata majibu ya uhakika na ya ukweli, waulizaji waliridhika na kupongeza hatua iliyochukuliwa na viongozi hao kutenga muda wao kuwasikiliza.

Vilevile, maabara za masomo ya sayansi ya Bulinga Sekondari yametembelewa. Sekondari hii kwa sasa inazo maabara mbili zilizokamilika na zinatumika (Chemistry & Biology). Ujenzi wa Maabara ya Physics unakamilishwa.

"Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini na viongozi wao wa ngazi zote wanaishukuru sana Serikali, chini ya uongozi mzuri wa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutupatia fedha za utekelezaji wa miradi yetu ya maendeleo."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news