Rais Dkt.Samia ateua mabalozi

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan amewapangia vituo vya kazi Mabalozi wakiwemo mabalozi wateule aliowateua tarehe 10 Mei, 2023.
Aidha, Mhe. Rais amewabadilisha vituo vya kazi Mabalozi wanne. 

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 11,2023 na Nkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,Zuhura Yunus. Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:

A. Mabalozi waliopangiwa vituo vya kazi:

i) Balozi Fatma Mohammed Rajab kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania nchini Oman. Balozi Rajab anachukua nafasi ya Balozi Abdallah 
Abasi Kilima ambaye amestaafu.

ii) Balozi Joseph Edward Sokoine kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Canada. Balozi Sokoine anachukua nafasi ya Balozi Dkt.Mpoki Ulisubisya ambaye mstaafu.

iii) Balozi Naimi Sweetie Hamza Aziz kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Austria.

iv) Meja Jenerali Ramson Godwin Mwaisaka (Balozi Mteule) kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Rwanda. Meja Jenerali Mwaisaka anachukua nafasi ya Balozi Meja Jenerali Richard Mutayoba 
Makanzo ambaye amehamishiwa Cairo, Misri.

v) Bw. Gelasius Gaspar Byakanwa (Balozi Mteule) kuwa Balozi wa Jamhuri ya 
Muungano wa Tanzania nchini Burundi. Bw. Byakanwa anachukua nafasi ya Balozi Jilly Maleko ambaye amestaafu.

vi) Bw. Habibu Awesi Mohamed (Balozi Mteule) kuwa Balozi wa Jamhuri ya 
Muungano wa Tanzania nchini Qatar. Bw. Mohamed anachukua nafasi ya 
Balozi Mahadhi Juma Maalim ambaye amehamishiwa Kuala Lumpur, Malaysia.

vii) Bw. Imani Salum Njalikai (Balozi Mteule) Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria. Bw. Njalikai anachukua nafasi ya Balozi Meja Jenerali Jacob Gideon Kingu ambaye amestaafu.

viii) Bw. Hassan Iddi Mwamweta (Balozi Mteule) Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ujerumani. Bw. Mwamweta anachukua nafasi ya Balozi Abdallah Saleh Possi ambaye amehamishiwa Geneva, Uswisi.

ix) Dkt. Mohamed Juma Abdallah (Balozi Mteule) kuwa Balozi wa Jamhuri ya 
Muungano wa Tanzania nchini Saudi Arabia. Bw. Abdallah anachukua nafasi ya Balozi Ali Jabir Mwadini ambaye amehamishiwa Paris, Ufaransa.

B. Mabalozi waliohamishwa vituo

i) Balozi Ali Jabir Mwadini kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa. Balozi Mwadini anachukua nafasi ya Balozi Dkt. William Shelukindo ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika 
Mashariki.

ii) Balozi Meja Jenerali Richard Mutayoba Makanzo kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri. Balozi Meja Jenerali Makanzo anachukua nafasi ya Balozi John Emmanuel Nchimbi ambaye anarejea nyumbani.

iii) Balozi Abdallah Saleh Possi kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Geneva, Uswisi. Balozi Possi anachukua nafasi ya Balozi Maimuna Tarishi ambaye amemaliza mkataba wake.

iv) Balozi Dkt. John Stephen Simbachawene kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uganda. Balozi Simbachawene anachukua nafasi ya Balozi Dkt. Aziz P. Mlima ambaye amestaafu.

Mabalozi wateule wataapishwa tarehe 16 Agosti, 2023 saa 05:00 asubuhi Ikulu, 
Chamwino jijini Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news