Rais Dkt.Samia azindua miradi mbalimbali kuelekea kilele cha Tamasha la Kizimkazi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan akipiga makofi pamoja na viongozi wengine mara baada ya kufungua Madarasa 6 ya jengo la Skuli ya Msingi Muyuni B tarehe 29 Agosti, 2023 Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi wengine wakati akikata utepe kufungua Chumba cha Kompyuta na ukumbi wa Mtihani wa Skuli ya Sekondari ya Muyuni B kwenye hafla fupi iliyofanyika Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi tarehe 29 Agosti, 2023. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi wengine katika picha ya pamoja na Walimu wa Skuli ya Msingi Muyuni B mara baada ya ufunguzi kwenye Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar tarehe 29 Agosti, 2023. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Skuli ya Maandalizi Tasani, Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar tarehe 29 Agosti, 2023. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna kuhusu Ujenzi wa Skuli ya Maandalizi Tasani, Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar tarehe 29 Agosti, 2023. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya kufungua Chumba cha Kompyuta na ukumbi wa Mtihani wa Skuli ya Sekondari ya Muyuni B kwenye hafla fupi iliyofanyika Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar tarehe 29 Agosti, 2023 katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati akikagua Madarasa ya Shule ya Msingi Muyuni B mara baada ya ufunguzi katika Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar tarehe 29 Agosti, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news