Serikali yasisitiza mshikamano mapambano dhidi ya Ukimwi

MBEYA-Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Mhe. Shamata Shaame Khamis amehimiza wananchi kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika Mapambano Dhidi ya Virusi vya UKIMWI nchini kwa kuendelea kuzingatia elimu inayotolewa kuhusu masuala hayo.
Mratibu kutoka Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Mathew Mwinuka akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Mhe. Shamata Shaame Khamis kuhusu shughuli zinazotekelezwa na programu hiyo wakati wa maonesho ya Nane nane yanayoendelea Jijini Mbeya.

Ametoa rai hiyo Agosti 6, 2023 alipotembelea Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu katika maonesho ya Kilimo Kimataifa yanayoendeleo Jijini Mbeya. Maonesho ya mwaka huu yamebebwa na Kauli mbiu inayosema “Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa mifumo Endelevu ya Chakula”

“Tunapaswa kuungana kwa pamoja, katika mapambano haya ya Virusi vya UKIMWI na kuhakikisha kila anayegundulika na maambukizi kuzingatia matumizi sahihi ya dawa, kujilinda na kulinda wengine,” alisema Mhe. Shamata
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa anayeshughulikia Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Prudence Constantine (wa kwanza kulia) akimkaribisha Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Mhe. Shamata Shaame Khamis (katikati mwenye sutio kijani) alipotembela katika Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane nane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya tarehe 6 Agosti, 2023, kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Anderson Mutatebwa.

Alitumia nafasi hiyo kukemea masuala ya unyanyapaa na kuhimiza jamii kuchukuliana na kuungana pamoja kupambana na maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI.

Akizungumzia kuhusu masuala ya maafa nchini Waziri Shamata aliikumbusha jamii kuzingatia taarifa za utabili wa hali ya hewa zinzotolewa na Mamalaka yua Hali ya hewa kwa lengo la kuchukua tahadhali dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza na kujikinga na maafa.
Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Mhe. Shamata Shaame Khamis akiweka Saini kwenye kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Ofisi yua Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) katika maonesho ya Nane nane Mbeya.

“Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha inailinda jamii yake katika majanga mbalimbali, ili kuendelea kuishi kwa furaha na usalama bila kukubwa na madhara yatokanayo na maafa nchini.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa anayeshughulikia Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Prudence Constantine akizungumza na waandishi wa habari alieleza kuwa, Ofisi imeendelea kutoa elimu kwa umma katika maonesho hayo juu ya uelewa wa matumizi sahihi ya bendera ya Taifa, kujua Nembo sahihi ya Serikali, pamoja na shughuli za uchapaji wa nyaraka na majukumu ya Baraza la Taifa la Biashara nchini.
Bw. Gilbert Mbwambo kutoka Tume ya Kudhibiti UIKIMWI nchini akimuonesha Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Mhe. Shamata Shaame Khamis Mkakati wa Tano wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI alipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu wakati wa maonesho ya Nane nane Jijini Mbeya.

“Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu yenye jukumu la kuratibu shughuli za Serikali na katika maonesho haya ya Kimataifa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi maarufu kama Nane Nane imeshiriki kwa kuhusisha baadhi ya Idara zake na taasisi ikiwemo,Idara ya Menejimenti ya Maafa, Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Nchini (TACAIDS), Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) na Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) kwa lengo la kutoa elimu kwa umma,”alieleza prudence.
Mratibu wa Maafa kutoka Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Henry Kissinga akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Mhe. Shamata Shaame Khamis kuhusu masuala ya Afya Moja walipotembelea katika banda la Ofisi hiyo katika maonesho ya Nane nane yanayoendelea Jijini Mbeya.

Aidha alieleza kuwa elimu zaidi itaendelea kutolewa katika masuala ya menejimenti ya maafa kuanzia ngazi ya Kijiji hadi Mkoa ili kuwajengea uwezo kukabiliana na maafa nchini.

Aidha kuhusu Program ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) alibainisha kuwa itaendelea kuratibiwa vizuri kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuimarisha na kuboresha utekelezaji wa programu hiyo.
Picha ya Pamoja ya baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) walioshiriki katika maonesho ya Nane Nane katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

“Ninakushukuru Waziri wa Kilimo Zanzibar Mhe. Shamata kwa kutembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu na kukiri kuridhishwa na huduma zinazotolewa hapa, tunaahidi kuendelea kutoa elimu kwa umma ili jamii iwe na uelewa wa pamoja juu ya shughuli za uratibu wa Serikali,”alisema Prudence.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news