Simba SC ujao ni msimu wetu

DAR ES SALAAM-Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amefurahi ubora wa kikosi alichonacho kuelekea msimu mpya wa mashindano 2023/24 huku akiweka wazi malengo yake kuwa ni kuchukua mataji ya ndani.

Robertinho amesema kikosi chake kina uwiano mzuri ambapo kwenye kila nafasi kuna wachezaji zaidi ya wawili wa kiwango cha juu.

Pia, Robertinho amesema aina ya kikosi alichonacho wanaweza kucheza mfumo wa aina yoyote na kupata matokeo chanya.

Mbali na hayo, Robertinho ameupongeza uongozi wa klabu hiyo kwa kusajili wachezaji bora huku akisema wamejipanga kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michuano ya ndani pamoja na kimataifa.

“Nimeridhika na kambi ya maandalizi nchini Uturuki. Tumekuwa na wiki tatu nzuri huku tukiwa na kikosi bora pia. Tuna wachezaji zaidi ya wawili kwenye kila nafasi.

“Naupongeza uongozi wa klabu kwa kufanya usajili huu mkubwa. Simba ni timu kubwa na tuna malengo ya kuchukua ubingwa wa ndani na kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa,”amesema Robertinho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news