Yanga SC yagawa dozi

DAR ES SALAAM-Yanga SC imeibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Friends Rangers katika mchezo wa kirafiki katika kambi yao iliyopo Avic Town ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni,Dar es Salaam.

Ushindi huo wa nusu dazeni ulitokana na mabao ya Clement Mzize, Crispin Ngushi,Stephane Aziz Ki,Hafiz Konkoni na Peodoh Pacome Zouzoua.

Katika mchezo mwingine wa kirafiki Yanga SC imetoka sare ya bila kufungana na JKU ya Zanzibar ndani ya uwanja huo huo.

Huu ulikuwa mchezo wa pili wa kujipima kwa mabingwa hao baada ya awali kuumana na Friends Rangers huku ikiibuka na ushindi mnono.

Aidha, kwa sasa klabu hiyo ya jijini Dar es Salaam imecheza mechi nne za kujiandaa na msimu chini ya kocha mpya, Miguel Angel Gamondi.

Mechi zilizotangulia ilikuwa ni dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ambao walitoka kwa ushindi wa 1-0 na dhidi ya Magereza ya jijini Dar es Salaam ambayo ilipigwa mabao 10-0.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news