Simba SC yatwaa Ngao ya Jamii

TANGA-Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam imetwaa Kombe la Ngao ya Jamii baada ya mtanange wa nguvu dhidi ya Yanga SC ya jijini humo.

Ni kupitia mtanange wa nguvu ambao umepigwa leo Agosti 13, 2023 katika Dimba la Mkwakwani jijini Tanga ambapo dakika tisini zilikwisha bila vigogo hao kufungana huku matufa yakiamua mshindi.

Katika mtanage huo, eneo la kiungo vita ilikuwa kubwa kwa timu zote zikipambania taji hilo la kwanza msimu wa 2023/24.
 
Simba SC imetwaa Ngao ya Jamii baada ya ushindi wa penalti 3-1 dhidi ya watani, Yanga kufuatia sare ya bila kufungana.

Unaweza kusema hii ni nyota njema kwa Simba SC ambao wamekuwa na ukame wa mataji kwa kipindi cha takribani miaka miwili.

Aidha, Ally Salum ndiye shujaa wa Simba SC baada ya kuokoa penalti tatu mfululizo za viungo Khalid Aucho, Pacome Zouzoua na beki Kouassi Attohoula Yao huku Stephane Aziz Ki pekee akifunga upande wa Yanga.

Muzamil Yassin na washambuliaji Leandre Willy Essomba Onana na Jean Othos Baleke ndiyo waliofunga penalti huku ya Saido Ntibanzokiza iliokolewa na kipa Djigui Diarra na ya Moses Phiri ikienda juu ya lango.

Awali,Azam FC imefanikiwa kumaliza nafasi ya tatu katika michuano ya timu nne ya Ngao ya Jamii baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Fountain Gate katika dimba hilo.

Prince Dube Mpumelelo dakika ya kwanza na kiungo chipukizi wa Kimataifa wa Tanzania, Abdul Suleiman Sopu dakika ya 42 ndiyo waliipa timu hiyo ushindi.

Nafasi hiyo wameipata baada ya kuangukia kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya tatu baada ya kufungwa 2-0 na Yanga SC kwenye mchezo wa Nusu Fainali wiki hii.

Aidha,Singida Fountain Gate ilitolewa kwa penalti 4-2 na Simba baada sare ya bila kufungana katika dimba hilo la Mkwakwani jijini Tanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news