Ayoub Lakred asaini miaka miwili Simba SC

DAR ES SALAAM-Mlinda mlango, Ayoub Lakred (28) raia wa Morocco amejiunga na kikosi cha Klabu ya Simba kutoka FAR Rabat kwa mkataba wa miaka miwili.
Lakred ambaye ni mlinda mlango kiongozi amewahi pia kuitumikia RS Berkane ya nchini Morocco.Lakred ana uzoefu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo tunaamini atakuwa msaada mkubwa.

Lakred ameiongoza FAR Rabat kushinda ubingwa wa Morocco msimu uliopita na kuifikisha Nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Lakred anakuja kuungana na Ally Salim, Hussein Abeli na Ahmed Feruz kipindi hiki mlinda mlango Aishi Manula akiendelea kuuguza jeraha lake. Uongozi wa simba SC unasema kuwa,unategemea uwezo wa Lakred utaimarisha lango lao kuelekea kuanza msimu mpya wa mashindano.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news