Tanzania, Cuba zakubaliana kuendeleza mchezo wa ngumi

HAVANA-Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Serikali ya Cuba kupitia Taasisi ya INDER ya nchini humo zimekubaliana kushirikiana katika eneo la kuendeleza mchezo wa ngumi.

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema kwamba, mabondia wa Tanzania watapata fursa ya kuweka kambi nchini Cuba ambayo pia itatoa makocha kuja kufundisha ngumi nchini na kubadilishana ujuzi.

Makubaliano hayo yamefikiwa Agosti 2, 2023 wakati Naibu Waziri wa wizara hiyo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ alipofanya mazungumzo na Raul Fornes Valenciano ambaye ni Makamu wa Rais wa Kwanza wa taasisi hiyo ya Kitaifa ya Michezo, Elimu na Burudani.

Aidha, taasisi hiyo ndiyo chombo kinachohusika na ukuzaji wa michezo, elimu ya viungo na burudani nchini Cuba huku ikiwa tayari ina mashirikiano na baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo Algeria ambapo hubadilishana uzoefu kwenye eneo la mchezo wa ngumi.Naibu Waziri Mwinjuma yupo nchini Cuba kwa ajili ya kuhudhuria maonesho ya kimataifa ya michezo ya Havana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news