CAF yakamilisha ukaguzi Tanzania

ZANZIBAR-Timu ya Wakaguzi ya utayari wa nchi za Tanzania, Kenya na Uganda kuwa wenyeji AFCON 2027, kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imehitimisha ukaguzi wao salama.

Zanzibar wamekagua Uwanja wa Amaan, Hospitali ya Mnazi Moja, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume pamoja na viwanja vingine vya mazoezi.

Ukaguzi huo umehitimika Agosti 2, 2023 jijini Zanzibar kwa kikao cha majumuisho kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu.

Akizungumza mara baada ya kikao hicho, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amezishukuru Serikali za nchi hizo kwa ushirikiano waliotoa kufanikisha ukaguzi huo ikiwemo nia ya kuomba kuwa wenyeji wa mashindano hayo.

“Ukaguzi umemalizika vizuri, kwa kweli wameona tupo ‘serious’ na kuna mambo ambayo wametuelekeza tuyafanye, kwa upande wetu kama Tanzania bara na Zanzibar yapo mengi yamefanyika kwa sababu wakandarasi wapo site na vitu vinaonekana.

"Wameelekeza hili jambo hili tulifanye kwa pamoja na wametoa siku 10 ili kukamilisha nyaraka zote zinazohitajika kulingana na maelekezo yao,”amesema Rais Karia.

Pia, Rais Karia ametoa rai kwa mataifa yote matatu kutekeleza kwa pamoja maelekezo yaliyotolewa ili kufikia lengo la Afrika Mashariki kuandaa mashindano hayo ambayo hayajawahi kufanyika katika ukanda huo na nchi hizo zinatakiwa kukamilisha miundombinu ya michezo itakayotumika kwenye mashindano hayo kabla ya Desemba 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news