Yaliyojiri ziara ya Waziri Dkt.Tax ofisi za AICC Arusha

ARUSHA-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) atembelea ofisi za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) kujionea utendaji kazi wa taasisi hiyo na kupanga kwa pamoja jinsi ya kutekeleza majukumu ya AICC kwa mwaka huu wa fedha na kuleta tija kwa Taifa. 
Mhe. Waziri katika ziara hiyo amezuru Chumba cha iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) iliyokuwa ikiendesha shughuli zake katika jingo la AICC , hospitali ya AICC, eneo litakalojengwa Kituo kipya cha Mikutano cha Kimataifa cha Mlima Kilimanjaro (MKICC) na kuzungumza na wajumbe wa bodi, menejimenti na watumishi wa AICC. 

Akizungumza na watumishi hao Mhe. Dkt. Tax amewataka kuhakikisha huduma wanazotoa zinaendana na mahitaji ya wakati uliopo ili kuhimili ushindani wa soko la biashara ya utalii wa mikutano na kuiwezesha taasisi yao kupata mikutano mingi zaidi. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akipokea shada la maua alipowasili katika Ofisi za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) jijini Arusha.

Mhe. Waziri pia amewapongeza watumishi hao kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuitangaza nchi pale wanapotokea kuandaa mikutano ya Kimataifa kama ilivyotokea kwa mkutano uliofanyika nchini hivi karibuni wa Wakuu wa Nchi za Afrika uliojadili rasilimali watu. 
Mkurugenzi Mtendaji wa AICC Bw. Emphraim Mafuru ( wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax alipowasili katika Hospitali za AICC jijini Arusha.

Katika ziara hiyo Dkt. Tax aliambatana na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa AICC walioongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Balozi Daniel Ole Njolay na Mkurugenzi Mtendaji wa AICC, Bw. Ephraim Mafuru. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax amembeba Mtoto wa kiume aliyezaliwa leo (tarehe 09 Agosti 2023) katika Hospitali ya AICC alipotembelea hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika Kituo cha AICC jijini Arusha.

Mhe. Dkt. Tax amefanya ziara ya siku moja ya kutembelea AICC kwa ajili ya kujadiliana nao na kuona ni jinsi gani wanaendana na mikakatiitakyoiwezesha AICC kuendelea kuwa Kituo bora cha Mkitano katika ukanda wa Afrika Mashariki. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisaini kitabu cha wageni kwenye Chumba cha iliyokuwa Mahakama ya Kimatifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) iliyokuwa ikiendesha shughuli zake katika jengo la AICC jijini Arushaalipozuru chumba hicho.

Ziara hii ni ya kwanza kwa Mhe Waziri tangu ateuliwa kushika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki mwezi Oktoba 2022. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha AICC alipotembelea eneo ambalo kitajengwa Kituo kipya cha Mikutano cha Kimataifa cha Mlima Kilimanjaro (MKICC) alipotembelea Ofisi AICC jijini Arusha.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya AICC Balozi Daniel Ole Njolay na Mkurugenzi Mtendaji wa AICC Bw. Ephraim Mafuru wakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax aliangalia kumbi mpya za mikutano zilizoongezwa katika Kituo hicho. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha AICC alipotembelea kituo hicho jijini Arusha.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na watumishi wa AICC jijini Arusha alipotembelea Ofisi za kituo hicho jijini Arusha.
Watumishi wa AICC wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax alipozungumza nao katika ofisi zao jijini Arusha.
Watumishi wa AICC wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax alipozungumza nao katika ofisi zao jijini Arusha.
Watumishi wa AICC wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax alipozungumza nao katika ofisi zao jijini Arusha.
Mwakilishi wa Watumishi wa AICC Bi. Catherine Kilinda akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa AICC tayari kumkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax alipotembelea ofisi za AICC na kuzungumza nao katika ofisi zao jijini Arusha.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akionesha zawadi aliyopewa na watumishi wa AICC alipotembelea ofisi za AICC na kuzungumza na watumishi wa AICC katika ofisi zao jijini Arusha.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na watumishi wa AICC alipotembelea ofisi za AICC jijini Arusha.

Kituo cha AICC ni moja ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Taasisi nyingine ni Chuo cha Diplomasia Dar es Salaam (CFR) pamoja na Mpango wa Hiari wa Kujitathmini wa Afrika (APRM).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news