Yanga SC yatinga Fainali Ngao ya Jamii

TANGA-Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imeichapa Timu ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam mabao 2-0 katika michuano ya Ngao ya Jamii.

Yanga SC ambao ni mabingwa watetezi wa ngao hiyo, wameupata ushindi huo usiku wa Agosti 9, 2023 katika dimba la Mkwakwani jijini Tanga.

Stephane Aziz Ki dakika ya 85 na Clement John Mzize dakika ya 89 ndiyo waliopeleka shangwe kwa wana Jangwani ambao kwa ushindi mnono.

Aziz Ki na Mzize walipeleka furaha hiyo Jangwani baada ya kutokea benchi kwa pamoja dakika ya 62, Aziz Ki akichukua nafasi za Crispin Ngushi na Mzize nafasi ya Farid Mussa wakati wa mtanange huo.

Kwa matokeo hayo, Klabu ya Yanga imeingia Fainali ya Ngao ya Jamii ambayo itachezwa Jumapili na itakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili baina ya Simba SC na Singida Fountain Gate FC.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news