Simba SC yapania kutwaa Ngao ya Jamii

DAR ES SALAAM-Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema, maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fountain Gate FC yamekamilika.

Robertinho amesema, wachezaji wapo kwenye hali nzuri kimwili na kiakili kuhakikisha wanapata matokeo chanya kwenye mchezo wa Agosti 10,2023 uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Ameongeza kuwa, Singida ni timu nzuri na imesajili wachezaji imara, lakini Simba ni kubwa na malengo yake ni kushinda taji.

“Kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo, wachezaji wapo vizuri. Tunafahamu itakuwa mechi ngumu, lakini tumejipanga kwa ajili ya ushindi ili tutinge fainali.

“Nafurahi kuona wachezaji wapya tuliowasajili wakiingia kikosini na kufanya vizuri. Juzi Willy Onana na Fabrice Ngoma walifunga mabao na wote ni wageni, hilo ni jambo zuri,”amesema Robertinho.

Kwa upande wake mlinzi wa kulia, Shomari Kapombe amesema wanategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Singida, lakini wapo tayari kupambana kwa ajili ya timu.

“Ngao ya Jamii ina maana kubwa kuichukua kwa sababu inakupa ramani kuelekea msimu mpya wa ligi utakavyokuwa. Tunajua utakuwa mchezo mgumu, lakini tumejipanga kushinda,”amesema Kapombe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news