Ajali ya ndege yaua watalii wote, marubani

BRASILIA-Ndege iliyokuwa imebeba watalii imeanguka huko Barcelos, Brazil na kusababisha vifo vya watu 14, kwa mujibu wa CNN Brasilia.
Picha na newsroompost.

Meya wa jiji hilo alithibitisha ajali hiyo kwa CNN Brasil siku ya Jumamosi.Ndege hiyo ilikuwa imebeba watalii 12, pamoja na marubani wawili, CNN Brasil iliripoti. "Hakuna walionusurika,"vyombo vya Ulinzi na usalama nchini Brazil vilinukuliwa.

“Abiria walikuwa wakienda eneo hilo kufanya mazoezi ya kujivinjari na ajali ilitokea kutokana na hali mbaya ya hewa. Mvua ilikuwa ikinyesha sana wakati wa kutua,” CNN Brasilia ilifafanua. Aidha, maafisa wa Serikali hawakutoa maelezo kuhusu uraia wa watu waliofariki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news