DC Mkasaba awashukuru madaktari, atoa wito

ZANZIBAR-Mkuu wa Wilaya ya Kusini, Rajab Yussuf Mkasaba amawaomba wahisani wa maendeleo kuzidi kutoa misaada yao itakayoinufaisha jamii moja kwa moja ikiwemo Sekta ya Afya.

Mheshimiwa Mkasaba ameyasema hayo huko katika Hospitali ya Wilaya Kitogani alipokuwa akizungumza na wataalam wa upasuwaji kutoka nje ya nchi waliotoa huduma za upasuaji katika hospitali hiyo.

Aidha, pamoja na kuwashukuru kwa huduma zao walizozitoa, Mkuu huyo wa wilaya amesema, wanaanchi wa wilaya hiyo pamoja na wilaya za jirani wamesifu huduma nzuri walizozipata.

Mheshimiwa Mkasaba amesema yeye binafsi ameridhishwa na itoaji wa huduma hizo ambazo hapo awali zilikuwa zikipatika Mnazi Mmoja, lakini sasa huduma hizo zinatolewa katika Hospitali ya Kitogani.

Pia, Mheshimwa Mkasaba amesema, Serikali ya Awamu ya Nane chini ya Rais wa Zanziba na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi inaendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya ili wananchi waweze kupata huduma bora iwe mijini na vijijini.

Hata hivyo, kupitia hafla hiyo, Mheshimiwa Mkasaba alitoa vyeti kwa madaktari hao kwa kutambua mchango wao mkubwa katika utoaji huduma bora hospitalini hapo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news