DED wa Busega, Veronica Vicent Sayore asimamishwa kazi

DODOMA-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa (Mb) amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Busega mkoani Simiyu, Veronica Vicent Sayore kuanzia leo Septemba 22, 2023 ili kupisha uchunguzi.

Mheshimiwa Mchengerwa amechukua hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko kuhusu utendaji kazi usioridhisha, kutokuwa na ushirikiano na viongozi wenzake pamoja na kutowashirikisha watendaji katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news