Hizi hapa bei mpya za mafuta Zanzibar leo

ZANZIBAR-Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imetangaza bei mpya za mafuta kwa mwezi Septemba 2023 ambazo zitaanza kutumika rasmi Jumamosi ya Septemba 9,2023.
Bei zilizotangazwa kwa mwezi Septemba ni kama zifuatazo, Petroli ni shilingi 2,950, Dizeli shilingi 3,012,mafuta ya taa shilingi 2,921 na mafuta ya ndege shilingi TZS 2,448 kwa lita.

Kwa mwezi Agosti, 2023 bei za mafuta zilikua Petroli shilingi 2,970, Dizeli shilingi 2,843, mafuta ya taa shilingi 2,921 na mafuta ya ndege shilingi 2,365.

Bei hizo zimetangazwa Septemba 8,2023 katika Ofisi za ZURA zilizopo Maisara na Meneja wa Kitengo cha Uhusiano, Mbarak Hassan Haji kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu ZURA na kueleza sababu za kuongezeka bei za dizeli na mafuta ya ndege ni kuongezeka bei hizo katika soko la Dunia kwa asilimia 21 na gharama za bima na usafirishaji kwa asilimia 62 ikilinganishwa na mwezi Agosti.

Aidha, Meneja huyo alitaja vigezo vinavyotumika na Mamlaka katika kupanga bei, ambavyo ni Wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta Duniani (Platts Quatations),

Gharama za uingizaji Mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam na Tanga,thamani ya Shilingi ya Tanzania kwa Dola za Kimarekani, Gharama za Usafiri, Bima na ‘Premium’ hadi Zanzibar, Kodi na Tozo za Serikali na Kiwango cha faida kwa Wauzaji wa Jumla na Reja Reja.

Mamlaka hutangaza bei za mafuta tarehe 8 ya kila mwezi ambapo hutoa wito kwa wananchi kununua mafuta katika vituo halali vya mafuta na kudai risiti za kielektroniki kila wanaponunua mafuta.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news