Hongereni sana,mkachape kazi-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameupongeza uongozi mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kufuatia kuteuliwa kwao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akizungumza na Uongozi mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliongozwa na Mhe.Januari Makamba (wa pili kulia) alipofika Septemba 11, 2023 Ikulu jijini Zanzibar kujitambulisha na Ujumbe wake. (Picha na Ikulu).

Rais Dkt.Mwinyi alitoa pongezi hizo Septemba 11, 2023 Ikulu jijini Zanzibar alipozungumza na viongozi hao
waliofika kujitambulisha.

Mheshimiwa Rais aliwasifu kwa kuteuliwa kwao na kueleza ni moja kati ya wizara muhimu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoibeba nchi nje ya mipaka yake.

Pia, Rais Dkt.Mwinyi aliwahakikishia ushirikiano wa kutosha uongozi huo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kueleza Serikali inaridhirishwa na ushirikiano wa kiutendaji unaoupata.

Ni kutoka kwa taasisi za Serikali za Jamhuri ya Mungano Tanzania hasa kwa taasisi za Muungano na sizizo za Muungano katika kuweka ufanisi wa utekelezaji wa shughuli za Serikali zote mbili.

Uongozi mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, Agosti 30 mwaka huu na baadaye kuapishwa Septemba mosi mwaka huu,Ikulu ndogo Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja kufuatia kufanya mabadiliko madogo ya Baraza lake la Mawaziri.

Walioteuliwa ni Waziri wa Wizara hiyo, Januari Yussuf Makamba ambae awali alitokea Wizara ya Nishati na Balozi Dk. Kennedy Gastorn alieteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshugulikia masuala ya Afrika Mashariki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news