Hospitali saba kutoa dawa za tiba asili nchini

DAR ES SALAAM-Jumla ya hospitaIi saba kuanza kutoa dawa za tiba za asili kwa wagonjwa wenye matatizo mbalimbali ya afya, mgonjwa atachagua dawa za kutumia kutokana na tatizo alilo nalo.
Hospitali hizo zitakazotoa dawa za tiba asili ni kulingana na kanda ni hospitali ya rufaa ya jijini Dar es Salaam ya Temeke, Morogoro, Dodoma General, Mwanza Sekou Toure, Arusha Mount Meru, Tanga Bombo na Mbeya

Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano la pili la kisayansi na Maonesho ya dawa za tiba asili Mkurugenzi wa Tiba Asili kutoka Wizara ya Afya, Profesa Pascal Rugajo amesema Hospitali hizo ambazo zimechaguliwa kwa kufuata kanda pia katika kuhakikisha yanafikia malengo wamesha toa mafunzo kwa watoa huduma watatu kwa kila hospitali.

"Tayari dawa zaidi ya 19 zitaanza kutumika kutibu, mgonjwa atafika kwa daktari ataonwa kwa njia ya kisasa mwisho ataambiwa kuna dawa za tiba asili na zawa za kizungu. Mgonjwa atachagua,"alisema Prof. Rugajo.

Amesema wameshaanza kutoa tiba kwa kutumia dawa za asili na mpaka sasa hakuna madhara yaliyojitoleza lakini wanaendelea kufanya utafiti ili kuhakikisha watanzania wanatumia tiba asili ambazo ni salama na zimethibitishwa zikiwa na mchango mkubwa katika kuendeleza tiba asili hapa nchini.

Ametaja baadhi ya magonjwa ambayo yanayoweza kupatiwa dawa za tiba asili katika hospitali hizo kuwa ni pamoja na vidonda vya tumboni, pumu, ngozi, upumuaji, magonjwa ya njia ya mkojo pamoja na magonjwa ya tumbo, kuungua moto na hata maumivu wakati wa hedhi.

Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Profesa Said Aboud amesema, taasisi yake inaendelea kukamilisha utafiti wa dawa ya asili ya kushughulikia tatizo la tezi dume kwa wanaume.

Amesema serikali inaendelea kufanya uwekezaji mkubwa wa afya, chini ya wizara ya afya na inapongeza jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kuendelea kuboresha sekta hiyo.

Aidha aliongeza kuwa kupitia kongamano hilo, wadau wa tiba asili, wakiwemo washiriki zaidi ya 200 watakuwa na maazimio ya namna ya kuboresha eneo la tiba asili, kutoa elimu lakini pia kuongeza utafiti ili kuhakikisha watanzania wanatumia dawa salama na zilizothibitishwa.

Amesema, wataendelea kuhakikisha kuwa tiba asili zinaendelezwa na tayari wapo madaktari, wauguzi pamoja na wafamasia ambao wamepatiwa mafunzo kuhusiana na huduma hizo shirikishi.

Kuhusu dawa za asili kuwa na madhara amesema, hakuna dawa isiyokuwa na madhara hata zile zisizokuwa za asili nazo zina madhara, kubwa ni mgonjwa kufuata masharti kutoka kwa wahusika.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Tiba asilia Wizara ya Afya, Dkt. Vumilia Liggie amesema, dawa za asilia katika Hospitali za umma zitaendelea kuongezeka kulingana na tafiti zinazofanyika

“Kwenye hizi hospitali ukimaliza mchakato wote wa kuonana na daktari, ukifika kwenye hatua za dawa, mgonjwa ana uamuzi wa kuchagua dawa aitakayo,” amesema Dkt. Liggie na kuongeza kuwa zipo nchi za nje kama China na India ambao wanaelndelea kutumia dawa hizo.

Kongamano hilo la pili la dawa asilia limewakutanisha wataalamu mbalimbali wakiwemo watunga sera, watumiaji wa dawa, watengenezaji, wanasayansi watafiti na Wanazuoni

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news