KMC FC yapata ushindi wa kwanza Ligi Kuu ya NBC

DAR ES SALAAM-KMC ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imefanikiwa kupata ushindi wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC.

Ni wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania kupitia mtanange uliochezwa Septemba 15, 2023 katika uwanja wake wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Awesu Awesu na Waziri Junior ndio waliofunga mabao mawili na kuifanya JKT Tanzania kuwa timu iliyoruhusu mabao mengi mpaka sasa kwenye Ligi kuu ya NBC kwa maana ya mabao saba sawa na KMC huku bao la JKT likifungwa na Edward Songo.

Ushindi huo umeipeleka KMC mpaka nafasi ya nane ikifikisha alama nne huku JKT ikisalia nafasi ya 10 nyuma ya Ihefu ya Mbeya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news