Lugha ya alama yajumuishwa kwenye utoaji huduma Muhimbili

DAR ES SALAAM-Hospitali ya Taifa Muhimbili imejumuisha lugha ya alama ili kutoa usaidizi kwa wagonjwa wenye tatizo la kusikia ili kuwaondolea changamoto za mawasiliano wakati wa kupata huduma za matibabu hospitalini hapa.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Masikio, Pua na Koo, Dkt. Aslam Nkya uamuzi huo umefanyika ikiwa ni jitihada za hospitali kuendelea kuboresha huduma kwa makundi mbalimbali miongoni mwa jamii na kuwapunguzia watoa huduma changamoto wanazokutana nazo wakati wa kuwahudumia wagonjwa hao.

“Kama mnavyotambua lugha ya alama ndio njia pekee ya mawasiliano kwa watu wenye changamoto za kusikia ndio maana uongozi umeona ipo haja ya kuwa na wataalam wa lugha ya alama ambao watakuwepo maeneo yote ya kutolea huduma na kuendelea kusambaza ujuzi kwa wataalam wote ili kurahisisha mawasiliano,”ameongeza Dkt.Nkya.

Dkt. Nkya amebainisha kuwa huduma hii inapatikana siku zote za kazi kwa wananchi wote waliopo ndani na nje ya Muhimbili ambao wanachangamoto hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news