Jean Baleke apiga hat trick, Simba yaipiga Coastal Union 3-0

DAR ES SALAAM-Mshambuliaji, Jean Baleke amefunga hat trick katika ushindi wa 3-0 waliopata Simba SC dhidi ya Coastal Union.

Ni kupitia mtanange wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa leo Septemba 21, 2023 katika Dimba la Uhuru lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Baleke awapatia waajiri wake Simba SC bao la kwanza dakika ya sita baada ya kumalizia pasi safi ya Clatous Chama akiwa ndani ya 18.

Aidha, dakika ya 10 Baleke aliwapatia bao la pili waajiri wake baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na mlinzi wa kushoto Mohamed Hussein.

Winga Hijja Ugando alioneshwa kadi nyekundu dakika ya 20 baada ya kumuumiza Henock Inonga ambaye alishindwa kuendelea na mchezo nafasi yake ikachukuliwa na Kennedy Juma.

Baleke alikamilisha hat trick kwa kufunga bao la tatu dakika ya 40 kwa mkwaju wa penati baada ya Luis Miquissone kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha alama tisa na kuungana na watani wao, Yanga SC ambao wanaendelea kuongoza Ligi kwa wastani wa mabao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news