Mashabiki wasusia tamasha la Burna Boy jijini Johannesburg

JOHANNESBURG-Mwimbaji wa Nigeria, Burna Boy ameahirisha tamasha lake la Johannesburg nchini Afrika Kusini kwa sababu ya mauzo kidogo ya tiketi.

Picha ya maktaba kwa hisani ya Christopher Polk/Variety/Shutterstock.

"Tunasikitika kutangaza kuahirishwa kwa tamasha la Burna Boy lililokuwa likitarajiwa kufanyika katika Uwanja wa FNB, Johannesburg mnamo tarehe 23 Septemba 2023. Tamasha hilo sasa litafanyika tarehe 16 Desemba 2023," ilieleza taarifa ya Ticket Pro.

Tamasha hilo lilipangwa kuanzisha Burna Boy After Tour, kulingana na tovuti ya Ticket Pro.“Uamuzi huu haukufanywa kirahisi na promota na umekuja kutokana na kutafakari kwa kina na kutathmini mambo mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa mauzo ya tiketi,”ilisema taarifa ya Ticket Pro.

“Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kwa wale ambao tayari wameshanunua tiketi,” iliendelea kueleza taarifa hiyo na kufafanua kuwa,

"Kwa mashabiki ambao hawawezi kuhudhuria tarehe hii, tumeanzisha chaneli maalum ya usaidizi kwa wateja. Tunaomba mashabiki watutumie barua pepe kwa info@ticketpros.co.za wakiwa na kumbukumbu ya tiketi ya Burna Boy na namba ya simu ya mkononi ili iweze kusaidia katika mchakato wa kurejesha fedha," iliongeza taarifa hiyo.

Vile vile, Ternary Media Group iliomba radhi kwa kuahirishwa tamasha hilo. "TMG inashukuru kwa msaada wa FNB Stadium, wasambazaji wetu, wadhamini na mashabiki wa Burna Boy katika kipindi hiki kigumu.Ikiwa wateja wangependa kurejeshewa fedha, TMG itashughulikia marejesho hayo kupitia Ticket Pro." (news24)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news