Mtoto Richard Mnkay amepotea, saidia kumtambua alipo

DAR ES SALAAM-Mtoto Richard Mnkay amepotea katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Kata ya Mji Mwema, Mtaa wa Kibugumo Msikitini au kwa Madadi, jana ijumaa tarehe 22/09/2023 aliondoka nyumbani kwa Mama yake Bi.Anneth Kiondo saa kumi jioni kwenda kucheza na wenzake nje hakuweza kurejea tena.

Jina lake ni Richard Mnkay, au “Rich” mvulana ana umri wa miaka 4, aliondoka nyumbani majira ya saa 10 jioni akiwa amevaa fulana ya mkato (car wash) ya rangi nyeupe , pensi nyeupe na raba nyeupe uwezo wake wa kujieleza ni mdogo sababu ya utoto lakini akiulizwa anaitwa nani? huwa anajibu anaitwa Rich.

Yeyote atakae muona au alimuona au amemukota sehemu tunaomba atoe taarifa kituo chochote cha polisi kilichokaribu na apige simu namba 0784842075 au 0715133709

Tunaomba ushirikiano huo mkubwa.

Asanteni

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news