Ninatambua umuhimu wa bima nchini-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, anatambua umuhimu wa mchango wa sekta ya bima kwa uchumi wa nchi na kujikinga dhidi ya majanga mbalimbali.

Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo Septemba 4, 2023 alipokutana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt.Baghayo Saqware na ujumbe wake waliofika Ikulu jijini Zanzibar.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amepongeza juhudi zinazofanywa na mamlaka hiyo kwa kuanzisha konsotia ya kilimo, pia na kuwataka kupanua wigo zaidi katika sekta za mifugo na uvuvi kwa kugusa wananchi wengi zaidi.

Naye Kamishna Dkt.Saqware amewatambulisha mabalozi wa mamlaka hiyo, kwa Mhe.Rais akiwemo Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Said, na Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Wanu Hafidh Ameir na Mhe.Japhet Hasunga ambao moja ya jukumu lao ni kutoa elimu ya uelewa wa bima kwa wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news