Mama Mariam Mwinyi azindua kambi ya matibabu, upasuaji bure

ZANZIBAR-Mke wa Rais wa Zanzibar ambaye ni Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF),Mama Mariam Mwinyi ametoa shukrani kwa uongozi wa Hospitali ya Kitengule, Tanlink Medical Tourism Agency.

Sambamba na wadau mbalimbali kwa kuandaa na kuratibu zoezi la utoaji wa huduma za afya za kibingwa ambazo zinatolewa bure kwa wananchi wa Zanzibar.

Mama Mariam Mwinyi ameyasema hayo Septemba 5, 2023 akizindua kambi maalumu ya matibabu na upasuaji iliyoandaliwa na Hospitali ya Kitengule, Tanlink Medical Tourism Agency kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Zanzibar.

Sambamba na Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) katika Hospitali ya Wilaya ya Kusini, Kitogani Mkoa wa Kusini Unguja.

Mama Mariam Mwinyi amesema, ni hatua muhimu kufanyika zoezi hilo katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa kuimarisha huduma za afya na kuzisogeza karibu kwa wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news