Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo na Uvuvi (AFDP) kuwavusha vijana

MOROGORO-Imeelezwa kuwa, uwepo wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo na Uvuvi (AFDP) itasaidia kuwezesha jamii kwa kupewa elimu juu ya ufugaji wa Samaki kwa njia ya kisasa huku ikiwajengea uwezo vijana kupitia mafunzo kwa vitendo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga akioneshwa vifaranga vya Samaki aina ya sato katika moja ya kisima kilichopo katika Kituo cha Kituo cha Kuendeleza Ukuzaji Viumbe Maji Kingolwira ambavyo vinaratibiwa na Ofisi yake chini ya Programu ya kuendeleza Sekta ya Mifugo na Uvuvi – AFDP mkoani Morogoro.

Hayo yamelezwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga wakati wa ziara yake ya kikazi kufuatili shughuli za utekelezaji wa Program hiyo, ambapo alitembelea katika Kituo cha Kuendeleza Ukuzaji Viumbe Maji Kingolwira kilichopo Mkoani Morogoro amesema, Ofisi yake ina jukumu kubwa na kuratibu program hiyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga akiangalia namna vifaranga vya Samaki vinavyoandaliwa katika maabara maalum Kituo cha Kituo cha Kuendeleza Ukuzaji Viumbe Maji Kingolwira alipotembelea kukagua utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi- AFDP inayoratibuwa na Ofisi yake.

Naibu Waziri alisema, uwepo wa programu hiyo unatoa fursa kwa kundi la vijana kupata ujuzi kupitia mafunzo kwa vitendo yanayotolewa na kituo hicho huku akiwaasa kuzingatia elimu wanayopata na kujali muda wanaoutumia ili kuwa na matokeo tarajiwa.
Kaimu Mkuu wa Kituo cha Kituo cha Kuendeleza Ukuzaji Viumbe Maji Kingolwira Bi. Gilness Frank akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera,Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga alipotembelea na kukagua utekelezaji wa Programu ya AFDP, inayoratibiwa na Ofisi yake.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa program ya AFDP katika kituo, Kaimu Mkuu wa Kituo cha Kuendeleza Ukuzaji Viumbe Maji Kingolwira Bi. Gilness Frank amepongeza juhudi za Serikali kwa kuendelea kuratibu uwepo wa program hiyo, huku akishukuru ufadhili wa Mfuko wa Kimataifa wa Kuendeleza Kilimo (IFAD) ambapo sekta ya uvuvi ni mnufaika.

“Programu hii imeendelea kuwa na tija kwetu tunaishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaendelea kufanikisha majukumu yake, imeendelea kuleta chachu kwa kuongeza uzalishaji wa Samaki, ajira katika mnyororo wa thamani na kuchangia kwenye uchumi pamoja na tasnia ya ukuzaji viumbe maji nchini kukua,” alisema Bi. Gilness.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali wanaofanya mafunzo kwa vitendo katika Kituo cha Kituo cha Kuendeleza Ukuzaji Viumbe Maji Kingolwira mkoani Morogoro.

Aliongezea kuwa kituo hicho kimeendelea kuwa mstari wa mbele katika utoaji wa huduma za ugani na mafunzo kwa vitendo kwa wanavyuo na watafiti kutoka Taasisi za ndani na nje ya nchi.

“Wadau wengi wamekuwa wakifika kituoni hapa kujifunza njia na kanuni bora za ufugaji wa Samaki, kupata vifaranga bora vya Samaki pamoja na kupata wataalam wa kutengeneza vyakula vya samaki."
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Kituo cha Kuendeleza Ukuzaji Viumbe Maji Kingolwira Bi. Gilness Frank wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo na Uvuvi ya AFDP kituoni hapo.

Alifafanua kuwa, jumla ya wafugaji 1319 wamenufaika kwa kupatiwa elimu ya ukuzaji viumbe maji, aidha jumla ya vifaranga 340630 aina ya sato vilizalishwa na kuwezesha kukusanya maduhuli jumla ya shilingi milioni 26, 171,000.
Afisa Uvuvi wa Kituo cha Kuendeleza Ukuzaji Viumbe Maji Kingolwira Bw. Ali Issa akitoa maelezo katika mabwawa ya kufugia Samaki katika kituo hicho kwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga alipotembelea kituoni hapo.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wanaofanya mafunzo kwa vitengo katika kituo hicho, Afisa Uvuvi wa kituo Bw. Ali Issa alipongeza ujio wa Naibu Waziri huo na kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kujali na kuwezesha shughuli za uzalishaji zinazoendelea kwa kuendelea kuunga mkono jitihada zao.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Programu inayoratibiwa na Ofisi yake ya AFDP, katika kituo cha Kituo cha Kuendeleza Ukuzaji Viumbe Maji Kingolwira mkoani Morogoro.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

“Kipekee nakushukuru sana kwa niaba ya vijana wenzangu, tunaahidi kuendelea kuwapa ujuzi vijana hawa ili wajifunze na kuleta tija katika sekta ya uvuvi nchini,” alisisitiza Ali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news