Tisa wahitimu darasa la saba, Mbunge Ole Lekaita afunguka

NA MATHIAS CANAL

MBUNGE wa Jimbo la Kiteto mkoani Manyara, Mhe.Edward Ole Lekaita amekoshwa na wanafunzi tisa ambao wamehitimu elimu ya msingi (darasa la saba) leo Septemba 22,2023 katika Shule ya Msingi Kititenebo ikiwa ni mahafali ya kwanza tangu kuanzishwa kwa shule hiyo.
Akizungumza wakati wa mahafali hayo ya kwanza ya shule hiyo amewapongeza wanafunzi tisa wakiwemo wasichana wanne na wavulana watano kwa uvumilivu wao, kwani walianza elimu ya msingi mwaka 2017 wakisomea chini ya mti,lakini hatimaye wamehitimu elimu ya msingi.

Mbunge Ole Lekaita amesema kuwa, huo ni uvumilivu wa hali ya juu kwani wasingekuwa wavumilivu wasingeweza kuhitimu elimu hiyo.
Amesema, katika jamii ya Kimasai mtoto kujitokeza na kusoma sio jambo jepesi, hivyo wanapofanya hivyo ni muhimu kutoa pongezi kwa wazazi/walezi, walimu pamoja na wanafunzi wenyewe.

"Mimi ninawapongeza na kuwaombea sana kwani ninaamini mtafika mbali kutokana na juhudi mliyoionyesha ya kuanza elimu yenu chini ya mti na sasa mmehitimu mkiwa kwenye madarasa mazuri.
"Wanafunzi wenzenu wanaobaki wametoa wosia kwenu kwamba hamjamaliza shule bali mmehitimu darasa la saba, bado safari yenu ni ndefu ya sekondari, vyuo vikuu na mtakuwa wanasheria, wabunge, madaktari na wataalamu katika nchi yetu."
Amewataka wanafunzi kuendelea kusoma kwa bidii kwani serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan inaendelea kuweka mazingira rafiki katika utoaji wa elimu ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya kujifunza na ufundishaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news